Zanzibar Bureau of Standards

TAARIFA KWA UMMA JUU YA BIDHAA YA MAFUTA YA VILAINISHI (ENGINE OIL) YALIYOINGIA KATIKA SOKO LA ZANZIBAR KINYUME NA UTARATIBU.

TAARIFA KWA UMMA JUU YA BIDHAA YA MAFUTA YA VILAINISHI (ENGINE OIL) YALIYOINGIA KATIKA SOKO LA ZANZIBAR KINYUME NA UTARATIBU.

Taasisi ya viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa Sheria ya Viwango ya Zanzibar namba 1 ya mwaka 2011. ZBS imeanza hatua za utekelezaji wa kazi zake rasmi mwaka 2012 ikiwa na jukumu la msingi la kuandaa viwango vya bidhaa zinazoingizwa na zinazozalishwa nchini na viwango vya huduma pamoja na kusimamia matumizi ya viwango hivyo. Lengo kuu la kazi za ZBS ni kulinda afya na usalama wa mtumiaji, kulinda mazingira pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Majukumu makuu ya ZBS ni kuandaa, kusimamia pamoja na kukuza matumizi ya Viwango vya Zanzibar, hivyo basi katika usimamizi wa ubora wa bidhaa ZBS imezuia bidhaa ya Mafuta ya vilainishi (engine oil) aina ya (DG OIL) Multipurpose Diesel & Petrol Engine Oil, SAE 40 API CC/SC katika ujazo wa lita 20 na Diesel Engine Oil SAE 40 API CP -4 yenye ujazo wa lita moja, ambayo baada ya kufanyiwa vipimo vya kimaabara mafuta haya ya vilainishi yamethibitishwa kuwa hayakidhi matakwa ya kiwango kilichowekwa na Taasisi ya Viwango(ZBS).

Kufuatia hali hiyo, ZBS inatoa taarifa kwa umma kwamba bidhaa hii ya kilainishi iliyoelezwa hapo juu, kwasasa imepigwa marufuku, usambazaji na utumiaji wake. Mfanyabiashara au muingizaji yoyote atakaebainika kuuza bidhaa hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na.1 ya 2011. ZBS inasisistiza kufanya ukaguzi na upimaji wa bidhaa hiyo kwa kutumia mfumo wa PVOC nje ya nchi ili kuondoa usumbufu.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz


CONTACTS
Zanzibar Bureau Of Standards
P.O. Box: 1136, Zanzibar
Tel: +255-24-2232225
Fax: +255-24-2232225
Email: info@zbs.go.tz
Website: www.zbs.go.tz


© Copyright 2021 - Zanzibar Bureau of Standards