Zanzibar Bureau of Standards

TAARIFA MUHIMU KWA WAINGIZAJI BIDHAA NCHINI

TAARIFA MUHIMU KWA WAINGIZAJI BIDHAA NCHINI

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) inawakumbusha wananchi wote kwamba kuanzia tarehe 01 Octoba 2021 bidhaa yoyote itakayoingizwa nchini (Zanzibar) ikiwa imo katika orodha ya bidhaa ambazo zinapaswa kukaguliwa kwa mfumo wa ukaguzi wa bidhaa nje ya nchi (PVoC) na bidhaa hiyo ikiwa imo katika jumla ya orodha ya bidhaa ambazo kwa sasa ZBS haijawa na uwezo wa kuzifanyia uchunguzi wa kimaabara (Testing) katika maabara za ZBS, ikaingizwa nchini pasi na kukaguliwa kwa mfumo huo wa PVoC, ZBS itachukua hatua zifuatazo kwa bidhaa hiyo:

i) Muingizaji wa bidhaa hiyo atalipishwa faini (Penalty) kwa mujibu wa kanuni na sheria ya Viwango ya Zanzibar.

ii) Kulipia gharama za uchunguzi, pia itachukuliwa Sampuli ya bidhaa hiyo na kupelekwa Maabara ya nje ya Zanzibar ambapo muingizaji atalazimika kutoisambaza wala kuiuza bidhaa hiyo hadi ZBS itakapopata majibu ya maabara kwa sampuli na kujiridhisha na ubora wake.

Orodha ya bidhaa ambazo zimo katika PVoC na ZBS kwa sasa haijawa na uwezo wa kuzifanyia uchunguzi katika maabara zake zinapatikana katika Tovuti ya ZBS www.zbs.go.tz au katika ofisi za ZBS Amani/Malindi/Bandarini Zanzibar. Na kwa Pemba, katika ofisi za ZBS Chakechake, Mkoani na Wete.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz


CONTACTS
Zanzibar Bureau Of Standards
P.O. Box: 1136, Zanzibar
Tel: +255-24-2232225
Fax: +255-24-2232225
Email: info@zbs.go.tz
Website: www.zbs.go.tz


© Copyright 2022 - Zanzibar Bureau of Standards