Zanzibar Bureau of Standards

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) inatoa taarifa kwa wananchi wote kwa ujumla hususan wafanyabiashara, waingizaji na wazalishaji wa bidhaa nchini kwamba, ZBS katika kutekeleza majukumu yake, inafanya ukaguzi wa bidhaa katika masoko, maduka, maghala na maeneo mengine mbalimbali ya bidhaa na kuchukua sampuli ya bidhaa husika na kuzifanyia uchunguzi wa kimaabara ili kutambua na kujiridhisha ubora wa bidhaa hizo.

ZBS inawatahadharisha kwamba bidhaa yoyote itakayobainika haikukidhi matakwa ya kiwango stahiki na kukosa kufuata taratibu za upatikanaji wa ubora wa bidhaa hiyo itachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kuendelea kuuzwa wala kusambazwa bidhaa hio kwa utaratibu unaofaa.

Hivyo, katika kuepukana na usumbufu na hasara inayoweza kutokea kwa wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa, ZBS inawaagiza wahusika kufika ofisi za ZBS Amani kwa kupatiwa viwango pamoja na utaratibu wa kupata Alama ya Ubora ili kulinda afya na usalama wa wananchi.

Zanzibar yenye bidhaa zenye viwango inawezekana.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz


CONTACTS
Zanzibar Bureau Of Standards
P.O. Box: 1136, Zanzibar
Tel: +255-24-2232225
Fax: +255-24-2232225
Email: info@zbs.go.tz
Website: www.zbs.go.tz


© Copyright 2022 - Zanzibar Bureau of Standards