Zanzibar Bureau of Standards

KATAZO LA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MIFUKO YA VITAMBAA (NON-WOVEN BAGS) ILIYO CHINI YA KIWANGO (GSM 70)

KATAZO LA UINGIZAJI, USAMBAZAJI NA UUZAJI WA MIFUKO YA VITAMBAA (NON-WOVEN BAGS) ILIYO CHINI YA KIWANGO (GSM 70)

Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) imeanzishwa kwa mujibu wa kifungu Na. 4(1) cha Sheria ya Viwango ya Zanzibar Na. 1 ya mwaka 2011. Majukumu makuu ya kuazishwa kwa ZBS, ni pamoja na kuandaa Viwango vya kitaifa vya Zanzibar pamoja na kusimamia matumizi ya Viwango hivyo.

ZBS inawakumbusha na kuwasisitiza wafanyabiashara wote wanaoingiza, wanaosambaza na wanaouza mifuko ya vitambaa (Non-Woven Bags) kuwa tarehe ya mwisho ya kuingiza, kusambaza na kuuza mifuko hiyo, ni tarehe 7/1/2020. Baada ya tarehe hiyo iliyotajwa ukaguzi utafanyika na atakayebainika kuingiza nchini, kusambaza au kuuza hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kutozwa faini kwa mujibu wa Sheria ya Viwango ya Zanzibar Na. 1 ya mwaka 2011.

ZBS inasisitiza kutumia bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika na ZBS.

Ahsante.

Imetolewa na:

MKURUGENZI MKUU
TAASISI YA VIWANGO ZANZIBAR.
S.L.P 1136,
NAMBARI YA SIMU: +255-24-2232225
Barua pepe: info@zbs.go.tz


CONTACTS
Zanzibar Bureau Of Standards
P.O. Box: 1136, Zanzibar
Tel: +255-24-2232225
Fax: +255-24-2232225
Email: info@zbs.go.tz
Website: www.zbs.go.tz


© Copyright 2021 - Zanzibar Bureau of Standards